Makala

Namna ya kujitengenezea sosi ya nyanya nyumbani (tomato sauce)

July 7th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa kutengeneza: Dakika 20

Nyanya kadhaa. Picha/ Margaret Maina

Vinavyohitajika

• nyanya kilo 1

• vitunguu maji viwili

• vinegar vijiko 3 vya chai

• sukari vijiko 2 vya chai

• chumvi kijiko kimoja cha chai

• maji ya moto kikombe kimoja cha chai

• majani ya giligilani

• mafuta ya kupikia

Kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.

Nyanya zilizokatwa vipande vidogovidogo. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Menya nyanya na vitunguu kisha vikate vipande vidogovidogo.

Saga mchanganyiko wa nyanya na vitunguu kwenye blenda hadi upate rojo.

Anza kuweka vinegar, sukari, chumvi, maji moto na mafuta ya kupikia katika blenda yako.

Saga kwa dakika kadhaa hadi uone imetokea rojo laini.

Namna nyingine

Tumia sufuria yenye nafasi kupika mseto huu.

Weka sufuria yako jikoni tia mafuta ya kupika, yakishapata moto, mwagilia rojo yako na kisha uanze kukoroga kwa dakika 30.

Baada ya hapo epua, sosi yako utakuwa tayari. Ifunge vizuri na kisha utumie kuandaa vyakula vyako.