Habari MsetoSiasa

Namtamani sana Mike Sonko, Diamond ni mtoto, Zari Hassan asema

July 15th, 2019 1 min read

Na PETER MBURU

MSOSHALAITI maarufu na pia mfanyabiashara kutoka Uganda Zari Hassan amekiri kuwa na mapenzi yasiyoisha kwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko, akisema amekuwa akimmezea mate kisiri na kuwa anamtamani sana.

Akizungumza na kituo cha redio kutoka Afrika Kusini, Zari alisema kuwa amekuwa akifuatilia shughuli za Sonko kwa muda sasa, hadi akaridhika kuwa ndiye mwanamume anayemfaa, kulingana na hadhi yake (Zari).

Akimlinganisha Sonko na mpenzi wake wa zamani, mwanamuziki kutoka Tanzania Diamond Platinumz, alimtaja Diamond kuwa mwenye utoto na mwenye tabia za kivulana. Lakini alisema Sonko ni mwanamume kamili kwa kuwa huwa anawasaidia wasiojiweza.

Alisema japo Diamond anapenda kujigamba na kuwa hajakomaa, Sonko ni mwanamume wa kuheshimika na mwenye tabia nzuri.

“Nataka kutangaza mapenzi yangu kwa Gavana mtanashati wa Nairobi Mike Sonko. Ndiye mwanamume ambaye nimekuwa nikimtamani kisiri kwa muda mrefu. Napenda gavana huyo mtanashati kwa kuwa ana tabia za kuheshimika. Hana tabia za kivulana kama huyo mtoto mwingine ambaye amekuwa akinifuata. Mkimuona Mike, tafadhali msalimieni na mumwambie kuna mtu anayemjali mahali,” akasema Zari.

Zari aliambia kituo hicho kuwa anapanga kutembelea Kenya kabla ya Desemba na kuwa anatumai atakutana na ‘mpenzi wake’ (Gavana Sonko) kwa mara ya kwanza, na wanywe kahawa pamoja.