Watu 8 wauawa katika mashambulizi baada ya ziara ya Matiang’i

Watu 8 wauawa katika mashambulizi baada ya ziara ya Matiang’i

BARNABAS BII Na GEOFFREY ONDIEKI

WATU wanane wameuawa katika mashambulizi tofauti Kerio na Samburu, siku chache baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i kutoa makataa ya wiki moja mashambulizi yakomeshwe.

Watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine watano wakapata majeraha mabaya, kwenye mashambulizi ya kupiza kisasi maeneo hayo.Miongoni mwao, sita waliuawa jana katika eneo la Chepkorowo, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, kwa mujibu wa Kamishna wa Kaunti Bw Ahmed Omar.

Watu wengine wawili waliuawa na wengine watano kujeruhiwa mashambulizi yalipozuka upya katika kijiji cha Nkoriche, Kaunti ya Samburu.Polisi walimkamata mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji hayo mapya eneo la Kerio.

Mshukiwa huyo kwa jina Kipsang Nyakone alinaswa akisaka matibabu ya majeraha ya risasi katika hospitali moja mjini Eldoret.Polisi walisema kwamba wanawafuata washukiwa wengine tisa. Mfugaji huyo aliuawa kwenye makabiliano makali kati ya wafugaji wa jamii za Marakwet na Pokot na kuzima mchakato wa kurejesha amani wa serikali, viongozi wa eneo hilo na viongozi wa kidini.

“Wafugaji hao kutoka jamii hizo mbili walishambuliana kwenye mto Kerio na kusababisha kifo cha mtu mmoja,” alisema kamanda wa polis wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Patrick Lumumba. Hakuna mifugo walioibwa kwenye shambulizi hilo.

Shambulizi la Samburu lilijiri chini ya saa kumi baada ya wafugaji wawili kutoka Marti kuuawa kwa kupigwa risasi na mifugo zaidi ya 500 kuibwa.Kamanda wa polisi kaunti ya Samburu Samson Ogelo alithibitisha kisa hicho na kusema waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali ya rufaa ya Samburu.

Bw Ogelo aliambia Taifa Leo kwamba maafisa wa polisi wametumwa kudumisha usalama.

  • Tags

You can share this post!

Machifu walivyopora mabilioni ya Covid

Polisi wazuia raia kuchota mafuta lori lingine likianguka