Michezo

Naomba unioe, kahaba amwambia Aguero

August 12th, 2019 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

MWEZI mmoja baada ya Sergio Aguero kufichua mpango wa kumfanya mwanamuziki maarufu mzawa wa Argentina, Martina ‘Tini’ Stoessel kuwa wake wa halali, kahaba Taylor Ward amekiri kurudiana na mwanasoka huyu wa Man City na Argentina.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Taylor alipakia mtandaoni picha alizopigwa kwa pamoja na Aguero walipokuwa wakiponda raha katika Kisiwa cha Sardinia, Italia na kusisitiza kwamba kubwa zaidi katika matamanio yake ni kufunga pingu za maisha na sogora huyo.

Aguero ambaye pia amekiri kutoka kimapenzi na mrembo Sofia Calzetti, alidhihirisha ukomavu wa penzi lake kwa Tini baada ya kuonekana wakibusiana peupe katika hafla ya kuadhimisha miaka 22 ya kuzaliwa kwa mrembo huyo aliyeandamana na mamaye mzazi, Mariana mwezi jana.

Aguero aliwahi kufunga pingu za maisha na binti wa Diego Maradona, Gianinna na wakajaliwa mtoto wa kiume kwa jina Benjamin kabla ya ndoa hiyo kusambaratika mnamo 2012.

Nyota huyu alianza kumtambalia Tini miezi michache baada ya kutemana mwanzo na Taylor, 21 aliyehusiana naye kwa siri. Kabla ya kupata hifadhi ya penzi lake moyoni mwa Aguero, Taylor aliwahi pia kumfungulia mzinga wake mwigizaji Sam Reece, 26, kabla ya tunda lake kumenywa na beki wa Everton, Mason Holgate, 22.

Baada ya kuzidiwa na baridi ya upweke tangu atemwe na kichuna Karina Tejeda mwaka jana, Aguero alianza kuburudishwa na mwanamitindo mzawa wa Italia, Zoe Cristofoli aliyewahi pia kutoka kimapenzi na Andrea Ceroli na mwanahabari Fabrizio Corona. Ceroli ni mshindi wa zamani wa shindano la Big Brother.

Zoe alianza kumfungulia Aguero buyu lake la asali mnamo Oktoba 2018, mwezi mmoja baada ya mvamizi huyo kuhusika katika ajali ya barabarani jijini Amsterdam, Uholanzi. Aguero alilidokoa tunda la Karina, 32, kwa miaka minne.? Karina ana mtoto mmoja, Sol aliyepatikana katika uhusiano wa awali na dume jingine.