Napiga chafya kupindukia, mbona?

Napiga chafya kupindukia, mbona?

Mpendwa Daktari,

Mimi hupiga chafya sana kila asubuhi na kila ninapokumbana na vumbi na harufu kali. Sikumbuki ni lini hasa nilipoanza kushuhudia haya, lakini nadhani ni tokea utotoni. Je, naweza kupata suluhu ya kudumu ili kukabiliana na tatizo hili? Nimetumia dawa nyingi lakini tatizo hili limesalia. Tafadhali naomba usaidizi.

Karis, Nairobi

Mpendwa Karis,

Yaonekana kana kwamba unakumbwa na tatizo linalofahamika kama allergic rhinitis. Hivi vinaitwa vichocheo na vinasababisha mshtuko kwa mfumo wako wa kupumua, na hivyo kumfanya mhusika kupiga chafya na wakati mwingine pua kuziba na kutokwa na kamasi.

Kwa kawaida hii huwa kwenye mfumo wa jeni wa mhusika, kumaanisha kwamba tatizo hili laweza kupitishwa kutoka kwa mzazi hadi kwa watoto, na hivyo haliwezi kukabiliwa.

Inahusishwa pia na hali zingine za mzio kama vile upele, kikohozi, kuashwa sehemu ya macho (allergic conjunctivitis) na maradhi ya pumu.

Mtu anaweza kukumbwa na hali moja kati ya hizi au zote kwa pamoja. Hali hii haiwezi kutibiwa lakini yaweza kudhibitiwa kwa kujiepusha na vichocheo kama vile baridi, vumbi, harufu kali, chavua na moshi, vile vile kutumia dawa za kukabiliana na mzio (anti-allergy medicines).

Vinyunyizi vya pua (Nasal sprays), pia vyaweza tumika kudhibiti hali hii.

You can share this post!

TIBA NA TABIBU: Mitandao ya kijamii yaanza kuteka watoto wa...

CHARLES WASONGA: Serikali itumie busara kuhusu suala kuu la...

T L