Napoli wakomoa Eintracht Frankfurt na kutinga robo-fainali za UEFA kwa mara ya kwanza katika historia

Napoli wakomoa Eintracht Frankfurt na kutinga robo-fainali za UEFA kwa mara ya kwanza katika historia

Na MASHIRIKA

VICTOR Osimhen alifunga mabao mawili na kusaidia Napoli kutinga robo-fainali za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kutandika Eintracht Frankfurt 3-0 mnamo Jumanne nchini Italia na hivyo kuwadengua kwa jumla ya mabao 5-0.

Chini ya kocha Luciano Spalletti, Napoli walishuka ugani Diego Armando Maradona wakipigiwa upatu wa kuwatamalaki wageni wao kwa mara nyingine.

Osimhen alifungulia Napoli ukurasa wa mabao mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya kupachika wavuni goli la pili katika dakika ya 53 kutokana na krosi ya Giovanni di Lorenzo. Piotr Zielinski alifanya mambo kuwa 3-0 kupitia penalti ya dakika ya 64.

Napoli wanapigiwa pia upatu wa kunyanyua taji la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) muhula huu na tayari wamejizolea pointi 68 kutokana na mechi 26 na wanajivunia pengo la alama 18 kati yao na nambari mbili Inter Milan kileleni mwa jedwali.

Kabla ya mechi, visa vya makabiliano makali vilishuhudiwa kati ya maafisa wa usalama na mashabiki wa Frankfurt waliopigwa marufuku kufika jijini Naples kwa ajili ya pambano hilo la marudiano la hatua ya 16-bora ya UEFA msimu huu.

Napoli sasa wamefunga mabao 25 katika UEFA msimu huu na kuvunje rekodi ya Benfica waliowahi kupachika wavuni idadi kubwa zaidi ya mabao katika msimu mmoja wa kampeni za kivumbi hicho.

Kwa kuangusha Frankfurt, Napoli sasa ndicho kikosi cha tatu cha Serie A baada ya Inter na AC Milan kufuzu kwa robo-fainali za UEFA msimu huu wa 2022-23.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Omanga ‘amcheka’ Raila kwa kutishia kumshtaki Rais

MCK yaunda sera ya kukuza uelewa wa habari

T L