Habari Mseto

Nashuku mke wangu anamgawia bosi wake asali, nishauri

April 12th, 2024 1 min read

Hujambo Shangazi,

Mimi nashuku mke wangu analala na bosi wake. Nina hasira sana.

Unajuaje kuwa mkeo analala na bosi wake? Ikiwa una ushahidi, muulize ili ujue ukweli. Lakini kabla ya kutaka kujua ukweli, jipe muda wa kupoa kwani hasira yaweza kufanya usababishe hasara.

Uzinifu kazini umeniletea sasa ugonjwa wa ajabu!

Nimeambukizwa kaswende baada ya kulala na kaka mmoja kazini. Nitamwambiaje mume wangu?

Unapaswa kujua kwamba ni hatari sana kushiriki tendo la ndoa kiholela bila kinga. Kando na kaswende, nenda upimwe kujua ikiwa uliambukizwa maradhi mengine ya zinaa na utibiwe. Ukiwa bado unapata matibabu, utashauriwa na daktari kutoshiriki tendo la ndoa, swali ni je, wakati huu wote utampa mumeo sababu ipi?

Mbona wote ninaoolewa nao huishia kuaga dunia?

Kila ninanopoolewa na mwanamume, anakufa. Nimelaaniwa?

Jamii tofauti huwa na imani mbalimbali kuhusu kifo cha mume hasa ikiwa kitatendeka zaidi ya mara moja. Itakuwa vyema kupata ushauri zaidi kutoka kwa wanaoelewa mila na itikadi za jamii yako kwani kama wasemavyo, mwacha mila ni mtumwa. Ikiwa huna hatia yoyote basi haupaswi kujilaumu kwa yale yaliyotendeka.

Mke anapenda ‘mchezo’ kupindukia, sina nguvu!

Mke wangu anapenda ngoma sana na wakati mwingi ananimaliza nguvu. Ni kawaida?

Naam ni kawaida kwa mwanamke kuwa na hamu kuu ya mahaba. Kama mumewe, itabidi ujikakamue katika nyanja hii kwani ikiwa hutamridhisha kuna uwezekano mkubwa kwamba ataanza kugawa huko nje. Fanya mazoezi na utambue mbinu nyingine salama za kukupa nguvu na kukuongeza ashiki ili uweze kumridhisha.