Nassir afunga majaa matatu ya taka

Nassir afunga majaa matatu ya taka

NA WINNIE ATIENO

GAVANA wa Mombasa Abdulswamad Nassir (pichani) amefunga rasmi jaa la Manyimbo, VOK na Kadongo huku zoezi la kukusanya taka hizo na kuzitupa katika jaa la Mwakirunge likianzishwa.

Bw Nassir alisema wakazi wa Mombasa watahamasishwa namna ya kugawa taka zao ili kutozikusanya kwa pamoja.

“Tunataka taka za plastiki ziwekwe kando. Tutaweka ua katika eneo la Manyimbo ili tuheshimu makaburi yetu. Tutawaita viongozi wa kidini waje wafanye maombo maalum,” alisema Bw Nassir.

Naibu wake Bw Francis Thoya alisema wawakilishi wa wadi watapewa jukumu la kuchagua eneo malaum ambapo taka zitakuwa zikikusanywa katika kila wadi.

“Hapo ndipo kaunti itakuwa ikichukua taka hizo na kuzipeleka eneo la Mwakirunge,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Wanaharakati wataka usalama uimarishwe Malindi

Mahakama yasita kutimua kampuni ya Joho bandarini

T L