Nassir ateua aliyekuwa katibu wa KMPDU kuongoza kamati ya afya Mombasa

Nassir ateua aliyekuwa katibu wa KMPDU kuongoza kamati ya afya Mombasa

NA FARHIYA HUSSEIN

GAVANA wa Mombasa, Bw Abdulswamad Nassir, amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wahudumu wa Matibabu na Madaktari wa Meno (KMPDU), Dkt Chibanzi Mwachonda, kuwa mwenyekiti wa kamati ya afya katika kaunti.

Dkt Mwachonda atasimamia kamati hiyo mpya iliyozinduliwa Alhamisi, huku Bw Mahmoud Noor, akiteuliwa kusimamia kamati ya masuala ya fedha.

Bw Nassir aliunda kamati hizo kupitia kwa amri kuu alizotia saini jana akisema hatua hiyo inalenga kusaidia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kaunti.

Kamati ya afya imepewa jukumu la kukagua utoaji huduma za afya ya umma hasa kuhusu usimamizi wa wafanyakazi wanaoajiriwa na serikali ya kaunti.

Kamati hiyo itatarajiwa kuandaa na kuwasilisha ripoti yake na mapendekezo kwa gavana ndani ya siku 30 zijazo.

Kwa upande mwingine, kamati ya fedha itatakikana kuwasilisha ripoti yake ndani ya siku 60.

Wanakamati watahitajika kujumuisha maoni ya wadau katika ripoti na mapendekezo yao.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yazindua rasmi mbolea ya bei nafuu

Arror, Kimwarer: Mashahidi sasa walia kutishwa

T L