Natembeya akosoa uongozi wa mtangulizi wake

Natembeya akosoa uongozi wa mtangulizi wake

Na OSBORN MANYENGO

GAVANA wa Trans-Nzoia George Natembeya ameukosoa uongozi wa serikali iliyotangulia kwa kutozingatia miundomisingi.

Akiongea na Taifa Leo afisini mwake mjini Kitale, alisema serikali ya mtangulizi wake ilikosa kuweka msingi bora wa kazi na mpangilio wa mji.

Natembeya alisema masoko yamejengwa bila kuwa na mpangilio kamili, akidai pia mji huu wa Kitale kukosa vyoo bora. vya umma.

Akiwataka mawaziri wake kuhakikisha kila kitu katika wizara zao kimewekwa kwa mipangilio.

Bw Natembeya alishangazwa sana kwa mji wa Kitale na viungani mwake kukosa maji safi ya mifereji na ilhali maji yanatoka vilima vya Cherangany.

“Mijengo mingi imejengwa yakiwemo masoko bila kufuata utaratibu unaofaa. Unapata vyoo vya watu binafsi lakini vya umma hakuna, hii ni kukosa mipangilio kamili na mwelekeo,” akasema.

Alitoa wito kwa waziri wa maji kaunti hiyo kuhakikisha wakaazi wa Trans-Nzoia wako na maji safi.

Alishangaa kuona kwamba eneo hili hutoa pesa zaidi za maji kuliko kaunti jirani ya Bungoma ambayo pia maji yake ni ya Trans-Nzoia NZWASCO, na inakosa maji.

  • Tags

You can share this post!

Polisi Fredrick Leliman ahukumiwa kifo kwa kuua wakili...

Wanahabari wapinga kuzuiwa kuingia bunge

T L