Naunga Raila kwa sasa ila macho yangu yako kwa urais 2027 – Kingi

Naunga Raila kwa sasa ila macho yangu yako kwa urais 2027 – Kingi

Na MAUREEN ONGALA

GAVANA wa Kilifi Amason Kingi amewakosoa wanasiasa ambao wanapinga hatua yake ya kubuni chama cha PAA akisema ni mbinu yake ya kujivumisha ili ifikapo 2027, awanie kiti cha urais.

Bw Kingi ambaye anakamilisha muhula wake wa pili uongozini Jumamosi alisema kuwa chama hicho kinaunga azma ya urais ya kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga kikilenga kushinda viti vingi vya uongozi katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

“Tunaunga mkono Raila kwa masharti kuwa lazima aitikie amri yetu. Iwapo ataenda kinyume cha matakwa yetu, tutamuuliza maswali. Mara hii tuna chama chetu na hatutaunga mkono vyama vingine,” akasema Bw Kingi.

Alikuwa akizungumza katika kituo cha kibiashara cha Matanomane, eneobunge la Ganze ambapo alisisitiza kuwa kubuniwa kwa chama cha PAA ni mwanzo wa safari yake ya kuingia ikulu 2027.

“Ninataka kuwaeleza wakazi wa Kilifi na Wakenya kuwa mimi siendi popote. Safari ya kuingia ikulu 2027 imeanza kwa kubuniwa kwa PAA. Inashangaza kuwa wanasiasa ambao wananipinga ndio wale ambao wamekuwa wakipigia upato chama cha Wapwani kibuniwe,” akaongeza.

Gavana huyo amekuwa akikashifiwa na baadhi ya wanasiasa wa eneo la Pwani kwa kuzua mgawanyiko kupitia kuendeleza maasi dhidi ya ODM ambayo ni maarufu sana katika eneo hilo la Pwani.

  • Tags

You can share this post!

Mlima wabusu Raila

Kocha Rangnick asema mvamizi Martial alikataa kuchezea...

T L