Habari Mseto

NCIC yaombwa kupeleka huduma mashinani

June 8th, 2024 1 min read

NA GEORGE MUNENE

WAKAZI wa Kirinyaga wanashinikiza Tume ya Kitaifa kuhusu Uwiano na Utangamano (NCIC) kuwatuma maafisa wake mashinani ili kupeleka huduma karibu na wananchi.

Walieleza kikao kilichofanyika mjini Mwea cha Kamati ya Bunge kuhusu Uwiano wa Kitaifa na Usawa kuwa maafisa wanapaswa kutumwa katika viwango vya kata ili kuboresha utoaji huduma.

Wakazi hao walilalamika kuwa wanalazimika kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za NCIC, wakisema suala hilo linafaa kushughulikiwa kwa dharura.

Mkazi kwa jina Brian Kamau, alisema japo NCIC ilizinduliwa zaidi ya miaka 15 iliyopita, watu wengi bado hawajaelewa majukumu yake kikamilifu.

Alitoa wito kuwepo uhamasishaji kuhusu wajibu wake kwa watu mashinani.