Habari Mseto

Ndani kwa kubaka msichana usiku mzima

June 2nd, 2020 1 min read

By WAWERU WAIRIMU

Mahakama ya Isiolo imemfunga mwanamume wa miaka 68 kwa kumbaka msichana miaka miwili iliyopita.

Gerald Murungi alipatika na hatia ya kumchafu msichana wa miaka kumi kinyume na sheria.

Korti ilisema kwamba msichana huyo alibakwa mara kadhaa  kati ya Juni 8 na Juni 13, 2018. Msichana huyo alisema kwamba mzee huyo alimdanyanya kuingia kwa nyumba yake alipokuwa akicheza.

Mzee huyo alimuomba msicha huyo amfulie nguo zake lakini akakataa. Mshukiwa huyo aliuamuru kuketi kwa kitanda, akamtoa nguo na kambaka huku akimfunika mdomo.

“Nilipokataa kumfulia nguo, alinifungia na akaniamuru niketi kwenye kitanda, akanitoa nguo na kunibaka usiku mzima,” alisema msichana.

Alikamatwa baada ya msichana huyo kuripoti kisa hicho kwa mjomba wake aliyejulisha polisi. Ripoti ya daktari ilionyesha kwamba msishana huyo alikuwa amebakwa.

Murungi alikataa mashtaka hayo na kudai kwamba yalikuwa madai ya uwongo.