Ndani miaka 30 kwa kumuua mfugaji

Ndani miaka 30 kwa kumuua mfugaji

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA wa kulinda wanyamapori amefungwa jela miaka 30 kwa kumuua mfugaji miaka nane iliyopita katika kitongoji duni cha Masai mtaani Embakasi, Nairobi.

Ijapokuwa alighairi kumuua Simon Koli, majaji wa mahakama ya rufaa Daniel Musinga na Kauthurima M’Inoti walisema Jonathan Lemiso ole Kini alikuwa amenuia kumuua au kumjeruhi mfugaji huyo ikitiliwa maanani matukio yaliyotangulia mauaji hayo.

Ole Kini alikuwa amekata rufaa kisha ikakataliwa.

Majaji hao walifutilia mbali hukumu ya kifo ambayo Jaji Roselyn Korir alikuwa amepitisha.

Majaji hao walisema mshtakiwa alienda kumsaka marehemu nyumbani kwake na kumchapa risasi ya tumboni.

Alipata majeraha kisha akampeleka hospitali ya Kijabe lakini akaaga akiendelea kupokea matibabu.

Bw Koli alikuwa alikuwa ameajiriwa na mshtakiwa kama mfugaji  kutunza mifugo nyumbani kwake kaunti ya Narok.

Majaji hao walisema mshtakiwa alimuua Koli pasi na sababu kamili ijapokuwa alikuwa anadai marehemu alitisha kumtwanga rungu.

“Jaji Korir hakutilia maanani kilio cha mshtakiwa kuwa angelikuwa na nia ya kumuua angelimpeleka hospurali,” walisema majaji hao.

You can share this post!

Misikiti yaagizwa ipeperushe bendera, ifunze waumini kuhusu...

Timu 50 za kimataifa kushiriki mashindano ya voliboli...

adminleo