Habari Mseto

Ndani miaka 30 kwa mauaji

July 3rd, 2020 1 min read

RUTH MBULA na FAUSTINE NGILA

Watu watatu walifungwa kifungo cha miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kuzua vita katika ugomvi wa ardhi Transmara.

Mahakama ya Kisii imewapata watu hao na hatia ya kuwaua watu wawili Aprili 2018 kutokana na ghasia za ardhi eneo la Mashangwa.

Jones Wambura, Tagane Mwita na Stephen Mahigara walijiwasilisha mbele ya Jaji Roseline Ougo.

Walishtakiwa pamoja na wengine ambao hawakuwa kwenye korti kwa kuwaua Samuel Magige na Samuel Nyamuroni katika Kijiji cha Kenyamangari.

Jaji Ougo alisema kwamba ushahidi uliowasilishwa kortini ulionyesha kwamba Wambura, Mwita na Mhigara waliwavamia Magige na Nyamuori  wakiwa na nia ya kuwaua ama kuwahumiza.

“Korti imeamuru kwamba watatu hao wafungwe miaka 30 kila mmoja kwa makosa mawili waliyotenda na wako na siku 14 za kukata rufaa,” alisema Jaji Ougo.

“Uchunguzi wa miili ya Magige na Nyamuroni hio ulionyesha kuwa ilikuwa imedungwa na kukatwa alisema,” alisema Dkt Peter Momanyi.