Habari Mseto

Ndani miaka 35 kwa kumuua mkewe

August 1st, 2020 1 min read

BRIAN OCHARO na FAUSTINE NGILA

Mwanaume wa miaka 50 kutoka Kilifi amefungwa miaka 35 baada ya kupatikana na hatia kumuua mkewe kufuatia mzozo wa nyumbani.

Riziki Karisa Yeri alimdunga bibiyake  Kadzo  Charo Chenje kisu mara kadhaa  baada ya kukosa kwenda shambani.

Kulingana na Mwanao Raeli Karisa babayake alimdunga mamayake  kifuani  na tumboni kutumia kisu cha jikoni..

“Nilipiga duru nduguzangu wengine wakakuja wakikimbia kuokoa mamangu,”alisema Bi Karisa.

Baada ya kutenda kitendo hicho Bi Karisa alisema kwamba babayake alijaribu kujitoa uai kwa kutaka kujidunga kisu.

Mwanao mwingine Bi Riziki Pili alishuudia kwamba aliamshwa na kelele kutoka chumbani kwa wazazi wake alipofika chumbani kwao alipata babayake akimdhulumu mamayao.

“Nilishuhudia mshukiwa akimdunga mwendazake tumboni na mguuni.alipomaliza alianza kumkakakata,”alisema shaidi huyo.I 

Alisema kwamba mamayao alikufia nyumbani kabla ya kupelekwa hospitali.

Afisa wa upelelezi aliyekuwa akishungulikia kesi alisema kwambaalipojulishwa kuhusu kisa hicho alituma gari kwenda kuchukua mwanaume huyo na mkewe lakini akfariki kwa maumivu.