Kimataifa

Ndani siku mbili kwa kusukuma rafikiye kutoka daraja la futi 50

May 15th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU
 
MWANAMKE wa miaka 19 kutoka Marekani ambaye alikiri kumsukuma rafikiye wa miaka 16 kutoka juu ya daraja katika eneo la kuogelea Jumatano alifungwa siku mbili jela.
 
Jaji wa mahakama hiyo Darvin Zimmerman alimfunga Tay’lor Smith, 19 kifungo cha siku mbili gerezani na siku 38 za kufanya kazi ya serikali.
 
Awali mwezi huu, Smith alikiri makosa ya utepetevu ambao ulisababisha majerahama mabaya dhidi ya rafikiye Jordan Holgerson.
 
Alikiri kumsukuma Jordan kutoka daraja hilo mnamo Agosti 7 katika eneo la Moulton Falls, kaskazini mashariki mwa Vancouver.
 
Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Youtube ilionyesha marehemu akisukumwa kutoka umbali wa futi 50, ambapo alivunjika mbavu na kupata majeraha mengine.
 
Smith kortini Jumatano alisema bado anapokea ushauri wa kisaikolojia kutokana na mshtuko aliopata kufuatia kisa hicho.
 
Holgerson naye alilia kortini alipokuwa akitoa ushahidi, akisema alidhani angekufa baada ya kuanguka majini.
 
“Tunaona bahati kubwa kuwa leo hii yuko hai,” akasema mamake mlalamishi Genelle Holgerson.