Habari

Ndindi Nyoro aachiliwa

September 10th, 2019 1 min read

Na NDUNG’U GACHANE

SENETA wa Murang’a Irungu Kang’ata amesema mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro – aliyekamatwa jana usiku – ameachiliwa baada ya maelewano na maafisa wa ngazi ya juu serikalini.

Seneta huyo amesema Jumanne asubuhi kwamba alikuwa ameshauriana na maafisa serikalini na ambao walikubali kutomshtaki mbunge huyo.

“Bw Nyoro hatashtakiwa na hakuna masharti kwa uamuzi huo. Hii ni baada ya kufanyika mashauriano baina yetu na maafisa serikalini,” Bw Kang’ata ambaye pia ni wakili wa kiongozi huyo ameambia Taifa Leo bila kuwataja maafisa hao.

Kwa mujibu wa polisi, Nyoro alifaa kukabiliwa na mashtaka ya kudhalilisha maafisa wa polisi, kukataa kukamatwa na kusababisha vurugu kanisani.

Nyoro alikamatwa Jumatatu usiku, muda mchache baada ya shoo ya runinga ambayo ilifanyika katika St James Cathedral, Murang’a.