NDIVYO SIVYO: Dhana ‘iko’ kwa maana ya ‘una’, mna, pana au kuna si sahihi – 4

NDIVYO SIVYO: Dhana ‘iko’ kwa maana ya ‘una’, mna, pana au kuna si sahihi – 4

NA ENOCK NYARIKI

KATIKA sehemu ya tatu ya makala haya, tulikuwa tumeanza kuangazia makosa mawili yanayojitokeza katika dhana ‘’iko’’ inapotumiwa kuonyesha mahali.

Kosa la kwanza ni la kingeli ambapo kiambishi {i} kimetumiwa badala ya {ku} cha mahali.

Kosa la pili linatokana na udondoshaji wa sehemu ya nomino. Kimsingi, anayetumia neno ‘iko’ kurejerelea mahali anatarajiwa kuuliza maswali mawili.

Swali la kwanza litarejelea mahali kwa kutumia viambishi mbalimbali vya ngeli ya mahali. Kwa mintarafu hii, swali hilo litajitokeza hivi: Huku kunauzwa au kunapatikana mboga?” au “Hapa panauzwa au panapatikana mboga?” Swali la pili litamrejelea anayeuza mboga. Kwa hivyo, msemaji anatarajiwa kuuliza: “Unauza mboga?”au “Wewe unauza mboga?”

Badala yake, mzungumzaji huyo ameamua kutumia njia ya mkato kwa kuuliza: “Iko mboga?’’

Dhana‘‘Iko’’ hutumiwa kama kitenzi kishirikishi kuonyesha uhusiano uliopo baina ya vitu na mahali. Dhana hii inapotumiwa kwa namna hii,sharti irejelee ngeli ya I-ZI au I-I bali si ngeli ya mahali.

Katika sehemu ya pili ya makala, tulieleza kwamba uhusishaji wa aina hii ndio baadhi ya wanasarufi hueleza kwamba vitenzi hivi hushirikisha vitu kihali, kitabia na kimazingira.

Alhasili, matumizi ya ‘iko’ kurejelea mahali ni njia ya mkato na yenye taksiri kisarufi ya kuwasilisha ujumbe. Iwapo mzungumzaji anataka kufahamu kuhusu kuwepo kwa kitu mahali fulani, basi anapaswa kutumia viambishi mbalimbali vya mahali kuwasilisha ujumbe huo.

Mifano: Huku kuna mboga? Hapa pana mboga? Humu mna mboga? n.k.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi wa Bondo wakesha wakisubiri matokeo ya urais

Ruto na Raila wafuatana unyounyo kwenye matokeo ya urais

T L