NDIVYO SIVYO: Kutofaa kwa matumizi ya ‘iko’ kwa maana ya ‘kuna’ au ‘una’

NDIVYO SIVYO: Kutofaa kwa matumizi ya ‘iko’ kwa maana ya ‘kuna’ au ‘una’

NA ENOCK NYARIKI

KATIKA sehemu ya pili ya makala haya tulitanguliza maana ya vitenzi vishirikishi.

Tulifafanua kuwa vitenzi hivi vinaweza kufasiliwa kwa njia tatu.

Tulikuwa tumeanza kuangazia fasili ya pili ya vitenzi hivyo ambapo tulieleza kwamba vinaonyesha ‘hali ya kuwa’. Tuliigawa hali ya kuwa katika viwango vitatu ambavyo ni kuwa na kitu, kuwa kwa kitu na kuwa katika hali.

‘Kuwa kwa kitu’ ni dhana ya uhusishaji ambapo uhusiano wa vitu na mahali unajitokeza. Mifano: Kitabu ki mezani; Amina yu darasani; Nyinyi m(u) rumande n.k.

Tunaposema kwamba fulani ni mgonjwa kauli hii inaibua dhana ya ‘kuwa katika hali fulani’.

Hali hiyo ndiyo inayoibuliwa na kauli: Juma ni mwizi, Ali ni mlevi; Kipchoge ni mrefu n.k.

Hatimaye, vitenzi vishirikishi huitwa hivyo kwa sababu huonyesha uhusiano baina ya maneno na mengine katika tungo. Dhana hii ndiyo baadhi ya wanasarufi huiita ushirikishaji. Ifahamike kuwa fasili tatu za vitenzi hivi zinazunguka dhima za vitenzi vyenyewe.

Katika utangulizi wa sehemu ya pili ya makala, nilieleza kuwa kauli zinazotumia dhana ‘iko’ kwa maana ya kuwepo kwa kitu mahali fulani zina kosa la ngeli na udondoshaji wa sehemu ya nomino.

Kimsingi, ‘Iko mboga?’ ni njia ya mkato ya kutaka kufahamu iwapo mboga zinapatikana mahali fulani.

Kutokana na swali lenyewe linajitokeza kosa la ngeli ambapo msemaji ametumia vibaya ngeli ya mahali. Ili kuzingatia upatanisho mwafaka wa kisarufi swali hilo lingejitokeza hivi: Kuna mboga?

YATAENDELEA

  • Tags

You can share this post!

Wawira ashindia Kenya medali ya shaba Birmingham unyanyuaji...

Afisa afungwa miaka 100 kwa kulawiti watoto

T L