Lugha, Fasihi na Elimu

NDIVYO SIVYO: Neno ‘lau’ katu halina maana ya ‘mfano wa’

January 11th, 2024 1 min read

Niliyakosoa matumizi ya namna hiyo ya ‘lau’ kwa kutoa sababu ambayo nitaitoa mwishoni mwa msururu huu.

Hata hivyo, baadhi ya walimu wangali wanawahimiza wanafunzi kutumia kiunganishi ‘lau’ jinsi tulivyoonesha hapo juu yamkini kwa kutofahamu kuwa si sahihi kisarufi.

Neno ‘kama’ huibua maana mbalimbali katika sentensi. Kwanza, huonesha mlingano au mshabaha uliopo baina ya vitu viwili. Kwa mfano: Chakula hiki ni kitamu kama asali.

Pili, huonesha mtegemeano wa kimasharti wa mambo ama hali mbili au zaidi. Nitaifafanua hoja hii zaidi baadaye kwa sababu ndicho kitovu cha mjadala huu.

Licha ya hayo, neno hilo hutumiwa katika ulinganishaji unaokusudiwa kukebehi, kusuta, kukejeli au kusisitiza wazo fulani. Kwa mfano: Unazitumia pesa zako ovyo kama kwamba hutaishi kuiona kesho!

Katika mojawapo ya mazungumzo yangu na Bwana Menge wa shirika la The Jomo Kenyatta Foundation, alitaka kufahamu iwapo ni sahihi kusema ‘kama kwamba’ kwa maana ya ‘kana kwamba’.

Aidha, alitaka kujua muktadha sahihi wa dhana hii. Nitalijibu swali hili katika sehemu ya pili ya makala haya.

Hatimaye, neno ‘kama’ hutumiwa kwa maana ya ‘kuwa’. Kumekuwepo na maoni ya kupotosha kuhusu matumizi ya ‘kama’ kwa namna hii katika majukwaa mbalimbali ya Kiswahili.

Haitakuwa nia yangu kuyajadili maoni ya aina hiyo hapa ila nitaje kuwa kauli ‘Hamisi ameteuliwa kama mwenyekiti wa bodi’ haina kosa kisemantiki.

MAKALA YATAENDELEA