Ndoto ya wanatenisi ya mezani wa Kenya kuwa Olimpiki yazimwa

Ndoto ya wanatenisi ya mezani wa Kenya kuwa Olimpiki yazimwa

Na GEOFFREY ANENE

Matumaini ya Kenya kuwakilishwa kwa mara ya kwanza kabisa kwenye Olimpiki katika fani ya tenisi ya meza yalizimwa wachezaji wake wote walipobanduliwa katika mchujo wa dunia jijini Doha, Qatar.

Brian Mutual, Josiah Wanders, Doreen Juma na Lydia Setey waliungana nje ya mashindano hayo na wachezaji wengine kutoka Bara Afrika ambao pia walionyeshwa kivumbi katika mchujo huo mgumu sana.

Katika kitengo cha wanaume cha mchezaji mmoja kila upande, Mkenya nambari moja Mutua alizidiwa maarifa 4-0 mikononi mwa Jancarik Lubomir kutoka Jamhuri ya Czech.

Wandera hakuwa na lake dhidi ya Tanviriyavechakul Padasak aliponyolewa bila maji na raia huyo wa Thailand 4-0.

Mambo hayakuwa tofauti katika kitengo cha kinadada pale mchezaji nambari moja nchini Juma alishindwa kumsimamisha Dvorak Galia kutoka Uhispania akilimwa 4-0.

Matumaini ya Mkenya kuwa katika raundi ijayo yalizimwa kabisa wakati Setey alipolishwa dozi hiyo ya 4-0 na Trigolos Daria kutoka Belarus.

Timu hiyo ya Kenya inatarajiwa nyumbani kutoka Doha mnamo Alhamisi usiku.

  • Tags

You can share this post!

Vijana wahimizwa kjiunga na mafunzo ya Taekwondo

Kinadada wa Kenya wafundisha wenzao kutoka Uganda jinsi ya...