Habari Mseto

Ndovu Tim mwenye pembe ndefu afariki akiwa na umri wa miaka 50

February 5th, 2020 1 min read

Na DIANA MUTHEU

NDOVU Tim – The Big Tusker – amefariki, shirika la kulinda wanyamapori nchini (KWS) limetangaza.

Kupitia akaunti ya mtandao wa Twitter, KWS imetangaza kuwa Tim alifariki mnamo Jumanne.

Tim alikuwa ndovu mzee sana mwenye pembe ndefu na alifariki akiwa na umri wa miaka 50 katika eneo la Mada katika mbuga ya wanyama ya Amboseli.

Mkurugenzi Mkuu wa KWS, Paul Udoto amesema kuwa shirika lilizuru eneo ambalo Tim alikumbana na kifo na mwili wake ukachukuliwa.

“Mwili wake umepelekwa katika makavazi ya Kenya (NMK) Nairobi na utachunguzwa na wataalamu wa wanyama kisha utahifadhiwa kwa ajili ya maonyesho,” akasema Bw Udoto.