Michezo

New Zealand majogoo wa raga South Africa 7s

December 16th, 2019 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

NEW Zealand ndio mabingwa wapya wa duru ya Afrika Kusini ya Raga za Dunia za msimu 2019-2020 baada ya kulima wenyeji Afrika Kusini 7-5 katika fainali kali mjini Cape Town, Jumapili.

Afrika Kusini, ambayo ilishinda duru hiyo yake mara ya mwisho msimu 2015-2016, ilitangulia kufunga mguso bila mkwaju kupitia kwa Justin Geduld mapema katika kipindi cha pili. Hata hivyo, Ngarohi McGarvey-Black kusawazisha na mguso ulioandamana na mkwaju kutoka kwa Akuila Rokolisoa.

Ufaransa iliridhika na nafasi ya tatu baada ya kuchapa mabingwa wa duru ya Afrika Kusini wa mwaka 2018 Fiji 29-24 katika muda wa ziada. Muda wa kawaida ulimalizika 24-24.

Timu ya Kenya almaarufu Shujaa ilimaliza ziara ya Cape Town katika nafasi ya saba kwa alama 11. Shujaa ya kocha Paul Feeney sasa ina jumla ya alama 15. Ilikuwa imezoa alama nne pekee katika duru ya ufunguzi mjini Dubai wiki moja iliyopita.

Jedwali la Cape Town 7s: New Zealand (alama 22), Afrika Kusini (19), Ufaransa (17), Fiji (15), Argentina (13), Ireland (12), Kenya (11), Scotland (10), Marekani (8), Uingereza (7), Canada (6), Australia (5), Samoa (4), Uhispania (3), Japan (2), Wales (1)

Msimamo wa Raga za Dunia baada ya duru ya Cape Town 7s:

New Zealand (alama 41)

Afrika Kusini 41

Ufaransa 29

Argentina 24

Uingereza 24

Fiji 23

Samoa 19

Australia 18

Marekani 18

Ireland 17

Kenya 15

Canada 13

Scotland 13

Uhispania 9

Wales 3

Japan 3