Afya na Jamii

Ngozi yangu inabambuka viganjani na kwenye nyayo

May 13th, 2024 1 min read

Mpendwa Daktari

Nimekuwa nikikumbwa na tatizo la ngozi kuambuka hasa viganjani na kwenye nyayo. Nini kinachosababisha hali hii?

Jessica, Nairobi

Mpendwa Jessica,

Ngozi yaweza kuambuka kutokana na kukaukiwa mwilini, kubabuka kwa jua (sunburn) au mwasho unaotokana na matumizi ya aina fulani ya sabuni, kukaa kwenye maji kwa muda mrefu au msuguano.

Tatizo hili laweza kabiliwa kwa kujipaka loshoni na kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha.

Hata hivyo, wakati mwingine hali hi yaweza kutokana na maambukizi, eczema, mzio, au matatizo katika kingamwili, au matatizo ya jeni hasa ikiwa ngozi inaambuka sana.

Itakuwa vyema ikiwa utatafuta ushauri wa mtaalamu wa ngozi ili uchunguzwe na matatizo kamili yatambuliwe, na utibiwe kabisa kabisa.