NGUVU ZA HOJA: Ufala aliouzungumzia Rais Ruto unaweza kupimwa kwa ratili?

NGUVU ZA HOJA: Ufala aliouzungumzia Rais Ruto unaweza kupimwa kwa ratili?

NA PROF IRIBE MWANGI

SIKU ya Jumatano nilikuwa ninaongea na kakangu mmoja kwa njia ya simu.

Baada ya mazungumzo kuhusu mambo ya kinyumbani, aliniuliza swali.

Sikuona hili kama jambo la kuwazia kwa kuwa ni kawaida kwa watu wengi kuniuliza maswali yahusuyo lugha, hasa ya Kiswahili.

Aliniuliza, “Je, ufala huweza kupimwa katika kilo?”

Sikuelewa kiini cha swali lake na nilidhani kuwa lililotokana na kutojua tu. Kwa sababu hiyo, nilimjibu kwa urefu.

“Ufala ni hali na ni neno lenye maana sawa na ubwege au upumbavu. Katika lugha, maneno kama haya huitwa dhahania kwa kuwa yanawakilisha vitu vya kufikirika tu. Kwa kuwa ni mambo ya kiakili, hayana mguso na kwa sababu hiyo vinavyowakilishwa havina uzito. Hivyo basi, ufala hauwezi kutiwa kwenye mizani kupimwa uzito wake,” nilimwambia.

Hata hivyo, kufikia jioni, nilibaini kwamba jibu nililompa kakangu lilikuwa na dosari.

Nilitenda kosa sugu ambalo aghalabu ndugu Matundura hutahadharisha dhidi yake; nilieleza maana ya maneno bila kumkutadhaisha.

Nilibaini hivyo baada ya kusikia sehemu ya taarifa aliyoitoa Mhe Rais Dkt William Ruto. Nilitambua kwamba katika muktadha wa matumizi yake, ni sahihi kutaja kuhusu uzito wa ufala.

Hii ni kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya lugha ya maandishi na lugha ya mazungumzo; lugha nathari na lugha ya kimafumbo.

Rais Ruto alitumia lugha ya mazungumzo na ya kimafumbo alipozungumza kuhusu “ufala ya kilograms nyingi sana.”

Mbali na kuchanganya ndimi, lugha hii hutumia tamathali kama vile sitiari inavyojitokeza hapa. Maana ya lugha basi hueleweka tu kutokana na muktadha wake.

  • Tags

You can share this post!

MIZANI YA HOJA: Jipangie jinsi ya kuendelea kuishi vizuri...

Wawili wakana kumvua nguo mhasiriwa wa wizi wa mabavu

T L