Ni kufa au kupona kwa Barca leo UEFA

Ni kufa au kupona kwa Barca leo UEFA

MUNICH, UJERUMANI

Na MASHIRIKA

LAZIMA Barcelona wapate ushindi leo usiku watakapokuwa ugenini kupambana na Bayern Munich kama wanataka kusonga mbele katika Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Ushindi katika mechi hiyo ya mwisho katika Kundi E utaweka hai matumaini yao kutinga hatua ya 16-bora kwenye michuano hiyo, iwapo Benfica watachapwa nyumbani na Dynamo Kyiv.Tayari Bayern wamefuzu kwa hatua hiyo, wakati Barcelona na Benfica wakiendelea kuwania nafasi ya pili.

Barcelona wanaingia uwanjani siku chache tu baada ya kuchapwa na Real Betis mwishoni mwa wiki katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), baada ya kwenda mechi sita bila kushindwa.

Mapema msimu huu kikosi hicho cha Xavi kilichapwa 3-0 ugani Camp Nou na Bayern Munich, hiki kikiwa kichapo cha tano kutoka kwa wapinzani wao baada ya kukutana mara sita.

You can share this post!

Masumbwi ya Jamal yang’oa nanga Kisumu

Klabu 12 kunogesha Jamhuri Cup Mombasa

T L