Nia yetu ni kuisaidia Kenya kumudu madeni – IMF

Nia yetu ni kuisaidia Kenya kumudu madeni – IMF

Na VALENTINE OBARA

SHIRIKA la Fedha Ulimwenguni (IMF) limejitetea baada ya kukosolewa na Wakenya mitandaoni kwa kuendelea kuipa serikali mikopo ya mabilioni ya pesa.

Mkurugenzi wa kitengo cha masuala ya Afrika katika shirika hilo, Bw Abebe Aemro Selassie, alisema serikali ya Kenya sawa na nyingine nyingi ulimwenguni, zinakumbwa na changamoto za kifedha ilhali kuna pingamizi kwa upandishaji ushuru.

Kulingana naye, mpango wa ukopeshaji uliopeanwa kwa Kenya si wa gharama kubwa, kwa vile ulizingatia jinsi tayari taifa limelemewa na madeni mengine mengi.

“Bila mikopo, serikali ingelazimika kupunguza madeni yake mara moja kwa kiasi kikubwa mno. Hili lingehitaji kupunguza matumizi ya fedha au kupandisha ushuru. Lakini kwa mtazamo wa kiuchumi, haya yote hayawezi kutimizwa wakati huu,” akasema.

Wiki mbili zilizopita, bodi kuu ya IMF iliidhinisha ombi la Kenya kupewa mkopo wa Sh257 bilioni, hatua iliyoibua hamaki kutoka kwa wananchi. waliolalamikia hali ngumu ya maisha licha ya mikopo mingine mengi ambayo serikali ilikuwa imechukua awali.

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Uamuzi kuhusu Sankara ulete mwanga mpya...

Tangatanga walia kuteswa na wandani wa Uhuru