Nice waadhibiwa vikali baada ya mashabiki kuzua vurugu katika mechi dhidi ya Marseille

Nice waadhibiwa vikali baada ya mashabiki kuzua vurugu katika mechi dhidi ya Marseille

Na MASHIRIKA

KLABU ya Nice imepokonywa alama mbili na sasa watalazimika kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Olympique Marseille baada ya mashabiki wao wa nyumbani kuvuruga mchuano wa awali wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Agosti 22, 2021.

Fowadi Dimitri Payet wa Marseille alirushiwa chupa ya maji ambayo naye aliiokota na kurejesha kwa mashabiki, tukio lililochochea mashabiki kujitoma uwanjani na kuzua rabsha.

Payet, mchezaji mwenzake Alvaro Gonzalez na kocha Pablo Fernandez wa Marseille pia wameadhibiwa.

Mechi ya marudiano kati ya Marseille na Nice sasa itachezwa bila mashabiki na katika uwanja usio nyumbani kwa kikosi chochote. Mbali na mchuano huo, Nice watapiga jumla ya mechi tatu nyinginezo bila mashabiki kuhudhuria.

Payet amepigwa marufuku ya mechi moja huku mwenzake Alvaro Gonzalez akipigwa marufuku ya mechi mbili. Kocha Pablo Fernandez wa Marseille amepigwa marufuku ya miezi tisa hadi Juni 30, 2022 bila kusimamia mchuano wowote uwanjani.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

AKILIMALI: Ufugaji nyuki washika kasi biashara ya asali...

Sheria maalum zawekwa kudhibiti sekta ya ujenzi Kiambu