Habari MsetoSiasa

Niko tayari kuelewana na Ruto – Raila

August 20th, 2018 2 min read

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa upinzani NASA Raila Odinga Ijumaa alisema kuwa yuko tayari kuweka muafaka wa maelewano kisiasa kati yake na Naibu Rais William Ruto katika juhudi zake za kuunganisha nchi.

Akiongea katika kijiji cha Kapsogeruk katika eneo bunge la Bureti wakati wa mazishi ya marehemu Mhandisi Joseph Chepkwony, Waziri huyo Mkuu wa zaman alisema safari ya kuwaunganisha Wakenya itajumuisha viongozi wote na hakuna atakayeachwa nje.

“Nimekuwa nikishirikiana kisiasa na marais wote wa Kenya kuanzia Marais wastaafu Daniel Moi, Mwai Kibaki na rais wa sasa Uhuru Kenyatta. Niko tayari kuweka muafaka wa maelewano na kila mtu akiwemo Naibu Rais William Ruto,” akasema.

Alieleza kuwa mpango wa maridhiano utasaidia kusuluhisha changamoto zinazowakabili Wakenya katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

“Hii ndio maana, Rais Kenyatta pamoja nami tumeamua kuzika tofauti zetu za kisiasa na kuendeleza mpango wa kuwaunganisha Wakenya. Kwa hivyo, sitaki kuacha mtu nje,” akasema Bw Odinga.

Alikuwa ameandamana na aliyekuwa Mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire na Mbunge Mwakilishi wa Homa Bay Bi Gladys Wanga.

Bw Odinga aliwataka watu wa jamii ya Wakalenjin kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi vinavyoendeshwa na serikali na kuondoa dhana kwamba ni watu wa jamii fulani wanalengwa.

“Usikimbie kumtetea mtu yeyote anayeshukiwa kushiriki ufisadi kabla ya mtu huyo kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka kubaini ikiwa ana hatia au la. Zingatia kuwa wakati mtu huyo alikuwa akiiba hakufanya hivyo pamoja nawe au kwa niaba yake,” akasema.

Akiguzia suala la kufurushwa kwa walowezi harama kutoka msitu wa Maasai Mau, Bw Odinga aliitaka serikali kutowafurusha watu ambao wanamiliki ardhi mbali na mpaka wa msitu.

“Kuhusu wale waliovuka mpaka wa msitu, lawama inafaa kuendea matajiri waliowauzia ardhi na ambao wanafaa kuadhibiwa kisheria,” akasema.

Bw Odinga alimsuta kiongozi wa wengi katika Seneti Kipchumba Murkomen kwa kujaribu kuingiza jina lake katika suala la kufurushwa kwa watu kutoka Mau.

“Alienda huko na kuanza kuwachochea huku akipaka jina langu tope kuhusiana na mchakato unaoendelea wa kuwaondoa watu wanaoishi Mau kinyume cha sheria. Ajue kwamba siku hizi mimi sio Waziri Mkuu na zoezi hilo linaendeshwa na watu wengine ambao sas wako serikalini,” akasem