Habari Mseto

Nilichungulia shamba boi wetu akioga na nilichoona mwili wangu unatetema

January 9th, 2024 1 min read

Mume wangu amesafiri kibiashara kwa wiki mbili. Juzi nilimchungulia mfanyakazi wetu wa shambani akioga ndani ya bafu. Nilichoona ni mimi tu najua. Tangu siku hiyo nikimuona moyo hunidunda na mwili kutetema. Usiku pia silali. Nifanyeje?

Hayo uliyataka mwenyewe! Ulidhani yataishia hapo na sasa yamekuwa balaa kwako. Kama hutaki kumkosea mume wako mpe likizo mara moja mjakazi huyo hadi mume wako arudi nyumbani.

Amekuwa akinipa pesa nikiwa chuoni, atanidai?

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Mpenzi wangu amekuwa akinipa pesa za matumizi. Lakini sitaki aendelee ili ifike wakati aanze kudai mambo nisiyotaka. Nishauri.

Huenda mpenzi wako anatumia pesa zake kwako akiamini utakuwa mke wake. Ni muhimu ajue wewe ni mpenzi wake tu kwa sasa. Pia mueleze wazi kwamba hatakudai chochote iwapo utabadili nia kuhusu uhusiano wenu.

Ex anataka nimzalie

Nina mume na watoto wawili. Lakini pia nina mpango wa kando ambaye ni mpenzi wangu wa awali. Tunapendana sana na ameniomba nimzalie mtoto mmoja. Nataka sana ila naogopa mume wangu atagundua.

Sitakubali kuwa mshirika wenu katika ulaghai huu wa kimapenzi unaotishia kuharibu ndoa. Kwa nini mwanamume huyo hakukuoa kama kweli mnapendana? Kama unajali ndoa yako achana na mapenzi haramu.

Kisima changu ni kipana ajabu, nahofia kukataliwa

Kuna jambo linanitatiza kuhusu mwili wangu. Nahisi kisima changu ni kipana sana. Naogopa hakuna mwanamume atakayeweza kunikubali kwa sababu hiyo.

Dhana yako ni potovu. Hilo kamwe si tatizo bali ni kawaida ya maumbile. Kuna watu wanene na wengine wembamba, warefu na wafupi. Huna sababu yoyote ya kushuku mwili wako.