Habari Mseto

Nilinaswa na gunia nzima la bangi, si misokoto 10 – Mshukiwa

June 5th, 2018 1 min read

Na Benson Matheka

MWANAMUME alizua kicheko katika Mahakama ya Kibera jana alipolaumu polisi kwa kumshtaki kwa kupatikana na misokoto 10 ya bangi badala ya gunia la kilo 90.

Fredrick Yusuf Shikanda alisema: “Ni kweli nilipatikana na bangi. Hiyo sipingi. Lakini ninashangaa kusikia eti nilikuwa na misokoto 10 ya thamani ya Sh200. Mheshimiwa, nilikuwa na gunia nzima la kilo 90 iliyojaa bangi.”

Madai yake yalimshtua kiongozi wa mashtaka Charles Mogaka ambaye alieleza mahakama kwamba hakuwa na habari kuhusu madai ya mshtakiwa.

Hakimu aliagiza afisa aliyemkamata kufika kortini leo kujibu madai ya mshtakiwa.