Michezo

Nina furaha tele kurejea Chelsea na niko tayari kwa kazi, asema Joao Felix


KIUNGO Joao Felix amejiunga na Chelsea kuchukuwa nafasi ya Conor Gallagher aliyehamia Atletico Madrid ya Ligi Kuu ya La Liga nchini Uhispania.

Felix amesaini mkataba wa miaka saba uliogharimu Sh7.5 bilioni, hii ikiwa mara yake ya pili kujiunga na Chelsea baada ya kuichezea kwa muda mfupi hapo awali kwa mkopo. Naye Gallagher amEjiunga na Madrid kwa kitita cha Sh5.5 bilioni kwa mkataba wa miaka mitano.

“Nina furaha tele kurejea Chelsea. Siwezi kusubiri kuanza kazi,” alisema Felix. “Ninaweza kuona nyuso zinazojulikana mara ya mwisho nilipokuwa hapa. Kitu ambacho ni kizuri kila wakati,” alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.

Gallagher ambaye huu ulikuwa mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake,  aLIjiunga na Chelsea akiwa na umri wa miaka sita na kuichezea mara 60 na kufunga mabao 10,  ameMshukuru kila mtu aliyemsaidia kutimiza ndoto yake.