Michezo

Nina mbinu ya kumzima Messi, asema Van Dijk

April 18th, 2019 1 min read

JOHN ASHIHUNDU

MERSEYSIDE, Uingereza

Beki tegemeo wa Liverpool, Virgil Van Dijk amesema wana mbinu maalum ya kumzima Lionel Messi watakapokutana na Barcelona kwenye nusu-fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Liverpool walijipata dhidi ya vigogo hao wa Uhispania kufuatia ushindi wao mkubwa wa 4-1 dhidi ya FC Porto, Jumatano usiku ugani Estádio do Dragão. 

Nyota wao matata, Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino kila mmoja alifunga bao katika mechi hiyo ambayo matokeo hayo yaliwapa ushindi wa jumla wa 6-1. Vile vile, Dijk alikuwa orodhani kwa waliofunga.

“Sijui itakavyokuwa, wacha tungojee tuone itakavyokuwa. Lakini kwa hakika, itakuwa mechi kubwa. Sote tumefurahia kufuzu kwa nusu-fainali na kila mtu anataka tuibuke mabingwa msimu huu, hilo pekee ndilo ninaloweza kusema kwa sasa. Mchango wa kila mtu utakuwa muhimu siku hiyo ikifika, ushindi sio wa mtu mmoja,” akasema.

Messi amekuwa akipewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari tangu afunge mabao mawili katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Manchester United na kuisaidia timu yake kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-0. Kufikia sasa, raia huyo wa Argentina amefunga mabao 45.