Habari

Nitazidi kutoa pesa, sijaiba za mtu- Ruto

May 24th, 2019 1 min read

Na PETER MBURU

NAIBU Rais William Ruto amesema kuwa ataendelea kutoa pesa katika makanisa na katika hafla za uchangishaji, akisema kuwa hatumii pesa za mtu.

Dkt Ruto amesema kuwa ni yeye anayejua anakotoa pesa hizo, kwani amekuwa mfanyabiara kwa zaidi ya miaka 30 na hivyo anajuana na watu wengi.

Naibu Rais aliendelea kusema hajachukua pesa za mtu, akishangaa ikiwa wanaolalamika wamepoteza pesa zozote.

“Nitaendelea kufanya yale ni ya kweli na hakuna mtu ambaye alipoteza pesa zake na akasema alikuta kwa akaunti yangu,” akasema Dkt Ruto.

Dkt Ruto alikuwa akizungumza katika kituo cha redio cha Kameme Alhamisi, ambapo alisema kuwa shida ya wanaomkosoa si pesa ila wanahisi wivu tu kwa kuwa anaendelea kujikuza vyema.

Kiongozi huyo aliendelea kusomea watu Biblia, kuonyesha kuwa alianzia chini miaka ya zamani na hivyo ndipo anapenda kuwasaidia watu wengine.