Njaa yawakosesha wanafunzi 1,603 umakinifu Mbeere

Njaa yawakosesha wanafunzi 1,603 umakinifu Mbeere

Na GEORGE MUNENE

ZAIDI ya wanafunzi 1,603 katika eneo pana la Mbeere, Kaunti ya Embu wanakabiliwa na baa la njaa na wanahitaji kusambaziwa chakula cha msaada kwa dharura.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Shirika la Maslahi ya Watoto (CWS), Peninah Nyarwai, watoto ambao wameathirika zaidi wanatoka katika shule za msingi za Rutumbi, Muthanthara, Ngiiri na Murukuci maeneobunge ya Mbeere Kaskazini na Mbeere Kusini.

“Kama shirika tutawasilisha mahindi na chakula cha msaada kwa wanafunzi wa maeneo haya ili kuwapunguzia makali ya njaa. Hata hivyo, serikali inafaa isambaze vyakula zaidi kuwanusuru ili waendelee kumakinikia masomo yao shuleni,” akasema Bi Nyarwai.

You can share this post!

JAMVI: Safari ya OKA, MKF imejaa visiki vingi

TAHARIRI: Taifa liige Kilifi kukabili mimba za mapema

T L