Habari Mseto

Njoo mtukamate, wasema Nyoro na Wahome

October 7th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Wabunge wawili Alice Wahome na Ndindi Nyoro wanatafutwa na polisi kuhusiana na vurugu iliyoshuhudiwa mji wa Kenol kaunti ya Murang’a  wamesema kwamba hawatatishwa na mtu yeyote.

Wawili hao ambao ni wafuasi wa nNaibu Rais William Ruto walisema kwamba hawako mafichoni na wako tayari kwa maswali ya mtu yeyote kama ilivyoagizwa na mkuu wa polisi.

Walisema kwamba wananyanyaswa na serikali kwa sababu ya msimamo wao wa kumuunga mkono Naibu Rais..

“Nasubiri polisi waseme ni lini wako tayari kunikamata hawatanifatuta.Hii ni siasa mbaya wanafanya lakini nashukuru wananchi kwani wanaona upuzi inayoendeshwa,” alisema Bw Nyoro mbunge wa Kiharu.