NMG yatoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi shuleni Kawangware

NMG yatoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi shuleni Kawangware

Na SAMMY KIMATU

WANAFUNZI zaidi ya 2,800 katika shule ya Msingi ya Kawangware Kaunti ndogo ya Dagoretti Mashariki, Nairobi wamepigwa jeki kielimu baada kupata msaada wa vitabu kutoka kwa kampuni ya Nation Media Group (NMG).

Kampuni ya NMG inayochapisha gazeti la Taifa Leo ilitoa msaada wa vitabu vya thamani ya Sh200,000 ilhali kampuni ya Bata ilipeana jozi za viatu kwa wanafunzi wote kuanzia chekechea hadi Darasa la Nane.

Wafanyakazi wa NMG waliongozwa na Mkuu wa Masuala ya Nje na Mauzo, Bw Clifford Machoka huku Meneja wa Kampuni ya Bata Nchini, Bi Jeddidah Thotho akiongoza wafanyakazi wenzake.

Akiongea kwenye hafla hiyo, Bw Machoka alisema nia ya NMG kuwasaidia watoto ni kubadilisha maisha yao kupitia elimu.

“Nia ya kampuni la NMG ni kubadilisha maisha ya wanafunzi kwa kupiga jeki elimu yao kupitia magazeti yetu ya Taifa Leo na Daily Nation,” Bw Machoka alisema.

Vile vile, Bw Machoka alisema NMG itatoa nakala za magazeti ya NMG ili wanafunzi wasome akifafanua kuwa kuna mambo mengi ya elimu ndani ya magazeti hayo.

You can share this post!

Haaland arejea kwa matao ya juu na kufungia Dortmund mabao...

UDA yaanza kuyumba

T L