Kimataifa

NOTRE DAME: Mtawa wa miaka 91 anauza ubikira kufadhili ujenzi

April 29th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMKE mtawa wa kanisa katoliki mwenye umri wa miaka 91 kutoka Ufaransa ametoa tangazo lisilo la kawaida kufuatia mkasa wa kuteketea kwa jengo la kihistoria la Notre-Dame, Jijini Paris, akisema sasa yuko tayari kuuza ubikira wake, ili kupata pesa za kujenga tena jengo hilo.

Antoinetter DeBasile, mtawa na bikira anasema kuwa anataka kuuza kitu anachothamini sana maishani mwake, ubikira, ili kupata pesa za kujenga jengo hilo tena.

Ajuza huyo ambaye alijiunga na utawa 1944 anasema yuko tayari kufanya chochote awezacho, ili kusaidia katika ujenzi wa kanisa hilo, ambalo limekuwa likiheshimiwa kuwa linalohifadhi historia.

“Nimejitunza maisha yangu yote kwa Mungu wangu na sasa ameniambia nijitoe ili kusaidia ujenzi wa jengo hilo,” DeBasile akaandikia vituo vya habari.

Mtawa huyo anasema kuwa tayari amepata bwanyenye kutoka Saudi Arabia ambaye yuko tayari kumlipa vizuri, japo akisema kuwa si mapenzi yake kulala na muislamu kwani hawapendi sana.

“Kwa hivyo ninaweza kumsubiri mtu wa dini ya Kikatoliki na anayemwamini Mungu,” akasema.

Alisema kuwa japo anahisi kama si kitu kifaacho, anaamini kuwa anafanya mapenzi ya Mungu.

Alikiri kuwa hajawahi kuona uume tangu alipozaliwa, ila kwenye intaneti na kuwa hajui jinsi tendo la ndoa hufanywa.