NPSC yateua kaimu DCI kushikilia kazi ya George Kinoti aliyejiondoa

NPSC yateua kaimu DCI kushikilia kazi ya George Kinoti aliyejiondoa

NA CHARLES WASONGA

TUME ya Kitaifa ya Huduma kwa Polisi (NPSC) imemteua Massa Hamisi Salim kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara Upelelezi wa Jinai (DCI) hadi mshikilizi kamili ya cheo hicho atakapoteuliwa.

Salim aliteuliwa Alhamisi, Septemba 29, jioni kupitia taarifa fupi iliyotolewa na tume hiyo.

“Tume ya NPSC imemteua Massa Hamisi Salim kama Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai kama kaimu hadi nafasi hiyo itakapojazwa ndani ya muda wa siku 14 zijazo,” ikasema taarifa hiyo.

Uteuzi huo unajiri siku chache baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) George Kinoti kujiuzulu mnamo Jumatatu wiki hii.

Habari kuhusu kujiuzulu kwamba ilitolewa na Rais William Ruto mnamo Jumanne alipotangaza orodha ya watu aliowapendekeza kuhudumu kama mawaziri katika serikali yake.

Tume ya NPSC ilitangaza kuwa  wazi nafasi ya Mkurugenzi wa DCI mnamo Septemba 29.

  • Tags

You can share this post!

Hisia mseto za wabunge kuhusu hotuba ya Rais Ruto

Tumaini la wadau wa utalii liko kwa serikali

T L