Habari Mseto

Nukuu za kuvunja mbavu zitakazofanya Mugabe kukumbukwa milele

September 6th, 2019 2 min read

Na MARY WANGARI

ALIYEKUWA Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alifariki hospitalini nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

Kiongozi huyo alianza kutawala Zimbabwe ambapo aliongoza kwa miaka 37 kabla ya kufurushwa mamlakani katika mapinduzi ya kijeshi miaka miwili iliyopita.

Kando na ujasiri wake na ukakamavu wa kusema alichofikiri ni sawa hata alipoonekana kuvuka mipaka, Mugabe atakumbukwa kwa kauli zake za aina yake ambazo baadhi ziliwavunja mbavu watu na zingine kuwaacha wakijikuna kichwa.

Hakukosa neno la busara kuhusu nyanja zote za maisha iwe ni elimu, jinsia, jamii au hata mahusiano ya ndoa jinsi ifuatavyo:

“Utaweza vipi kushawishi kizazi kijacho kwamba elimu ni ufunguo wa ufanisi wakati wanazingirwa na wahitimu fukara na wahalifu matajiri?” alihoji kuhusu elimu.

Kuhusu ubasha, hakuchelea kueleza hisia zake: “Tunauliza, alizaliwa kutokana na ushoga? Tunahitajhi kuendeleza kizazi chetu na kinatokana na mwanamke na la kwa ushoga. John na John, la; Maria na Maria, la. Ni waovu kushinda mbwa na nguruwe. Ninafuga nguruwe na nguruwe wa kiume anamjua yule wa kike.”

“Ikiwa rais Barrack Obama anataka niruhusu wanandoa wa jinsia moja nchini kwangu (Zimbabwe) ni sharti aje hapa ili nimwoe kwanza,” alisema.

“Ni vigumu kumroga msichana Mwafrika siku hizi kwa sababu kila unapopeleka unywele wake kwa mganga ama mwanamke asiye na hatia raia wa Brazil anashikwa na kichaa au kiwanda Uchina kinateketea,”

“Hakuna kinachomchanganya mwanamke kuliko kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamme mlofa ambaye ni stadi wa miereka kitandani,”

“Wanawake, ikiwa unaweza nyoa nyusi zake na kisha uzichore zirejee, usiitishe hela za salon, nyoa tu kisha uchore mtindo unaotaka,”

“”Takriban naira milioni moja kusomea kemia katika chuo kikuu cha kibinafsi Nigeria ilhali hakuna yeyote amevumbua kitu chochote, hata mafuta ya upako.”

Kuhusu wanaume wakware hakukosa ushauri:

“Ikiwa wewe ni mwanamume uliyeoa na unajipata ukivutiwa na wasichana wa shule, mnunulie tu mkewe sare ya shule,” alisema.

“Ikiwa mumeo anaenda nje ya ndoa usibishane naye dadangu kwa sababu hutashinda. Jinusuru kutokana na shinikizo la damu. Badilsha majina yote ya wanawake kwenye simu yake. Usifute nambari. Zichanganye Natasha umwite Lisa, Nikki umwite Grace. Subiri atakapopiga simu ama kuwatumia sms mmoja baada ya mwingine. Jiandalie kikombe cha kahawa na utulie, utanishukuru baadaye,”