Habari Mseto

Nyanza hatarini maafisa wa afya wakigoma

August 6th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Eneo la Nyanza liko kwenye hatari ya kukosa huduma za afya baada ya maafisa wa afya kugoma kwa madai ya kukosa kuongezwa mshahara na kutolindwa wakati huu wanapambana na virusi vya corona.

Madaktari wa Kaunti ya Siaya wamepeana notisi ya mgomo ya siku saba na kuamua kugoma Jumatatu wiki moja baada ya weNzao wa Kaunti ya Homa Bay.

Maafisa wa afya wa Kaunti ya Kisii walikua wameamua kufanya mgomo Jumanne lakini gavana wa kaunti hiYo James Ongwane akaahidi kwamba watalipwa Ijumaa wiki ijayo.

Maafisa hao wanalamikia kucheleweshwa kwa mishahara, kupandishwa cheo na kunyimwa vifaa vya kujikinga.