Habari za Kaunti

Nyeri: Wafanyakazi wa kaunti waagizwa kufunga baa zao

March 15th, 2024 1 min read

WAFANYAKAZI wa kaunti ya Nyeri wanaomiliki baa wamepewa notisi ya wiki moja kufunga biashara zao.

Akizungumza Ijumaa wakati wa kuidhinisha Mswada wa Kaunti wa Kudhibiti Vileo uliopitishwa na Bunge la Kaunti mwezi Februari na kuwa sheria, Gavana Mutahi Kahiga alisimamisha utoaji wa leseni mpya kwa wanaomiliki baa hadi mchakato wa uhakiki utakapokamilika.

“Hii ina maana kwamba katika kipindi cha wiki mbili zijazo, viongozi wote waweke ramani ya kila baa, namba za usajili, wamiliki na bidhaa zinazouzwa,” gavana Kahiga alisema.