Habari Mseto

Nyong'o apiga marufuku disko matanga

October 1st, 2020 1 min read

NA RUSHDIE OUDIA 

Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyongo’ amepiga marufuku sherehe za disko matanga kufuatia kuongezeka kwa virusi vya corona nchini.

Isipokuwa kwamba nchi inashuhudia kupungua kwa virusi vya corona Gavana  Nyong’o alisema kwamba virusi vya corona vinaendelea kuongezeka katika kaunti hiyo.

Ujumbe wake unajiri wiki moja baada ya kuongezeka kwa maaambukizi ya corona kaunti hiyo huku visa vingine vikiwa vya jela.

“Bado hatujatoka kwenye hatari ya corona, wiki mbili zilizopita tumeshuhudia kuongezeka kwa maambukizi ya corona kwenye jamii zetu,’ alisema.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Afya Alhamisi ilionyesha jumla ya maabukizi 495  na vifo nane kaunti ya Kisumu.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA