Nyoro ateua mawaziri wapya

Nyoro ateua mawaziri wapya

Na LAWRENCE ONGARO

GAVANA wa kaunti ya Kiambu Dkt James Nyoro tayari ameteua baraza lake la mawaziri huku wakisubiri kuidhinishwa rasmi na bunge la kaunti hiyo.

Kwanza naibu wake atakuwa ni Joyce Wanjiku Ngugi. Kulingana na baraza lake aliloteua, waziri wa fedha na mipango ni Bw Wilson Mburu Kang’ ethe.

Dkt Margaret Waithera Ruinge, ni waziri wa maswala ya umma na usimamizi.

Bw James Mutambo Maina ni waziri Wa ardhi, nyumba, na mipango.

Bw David Kimani Kuria ni waziri wa maji na mazingira.

Bi Mary Kamau ni waziri wa elimu na jinsia.

Bw John Mwangi ni waziri wa kilimo, mifugo, na uvuvi.

Bw Francis Kigo Njenga ni waziri wa biashara na utalii.

Dkt Joseph Murega ni waziri wa Afya.

Naye mhandisi Samuel Mugo Kimani ni waziri Wa Barabara na uchukuzi.

Baada ya uteuzi huo Dkt Nyoro aliwahimiza mawaziri hao kutekeleza wajibu wao kwa bidii .

“Natarajia kila mmoja wenu atatekeleza wajibu wake kwa bidii bila ubaguzi wowote,” alisema gavana huyo.

Uteuzi huo umeonyesha wazi ya kwamba wengi wa mawaziri wa zamani wametemwa na kuwaweka wapya.

Wakazi wa Kaunti ya Kiambu wanamatumaini makubwa kupata huduma bora kutoka kwa mawaziri hao wapya.

“Tumefurahi kusikia kuwa gavana Nyoro amewateua mawaziri wapya. Iwapo watatufanyia Kazi bila shaka tutafurahia sana,” alisema Bw James Gitau, ambaye ni Mfanyi biashara mjini Thika.

You can share this post!

CORONA: Magereza ya Thika yanyunyiziwa dawa

CORONA: Visa vyafika 122, mvulana wa miaka 6 afariki

adminleo