Nyota wa ‘Vuta Pumzi’ alifariki kutokana na kansa ya ubongo

Nyota wa ‘Vuta Pumzi’ alifariki kutokana na kansa ya ubongo

Na THOMAS MATIKO

MMOJA wa wanamuziki maarufu wa kizazi cha sasa, Christian Longomba, memba wa kundi la The Longombas alifariki Jumamosi kutokana na kansa ya ubongo.

Amekuwa akiugua ugonjwa huo kwa miaka sita hadi alipofariki akiwa na umri wa miaka 37. Kifo chake kilithibitishwa na kakake pacha, Lovy.Wawili hao wanakumbukwa kwa nyimbo zao kama vile, Dondosa, Makofi, Shikamoo, Vuta Pumzi miongoni mwa nyingine.“

Christian Hulu Longomba alifariki majira ya asubuhi jijini Los Angeles, jimboni California, Amerika (USA) baada ya kuugua kwa muda mrefu. Christian alipendwa na kuhusudiwa kutokana na kipaji chake kilichohusudiwa kote ulimwenguni,” akasema Lovy, ambaye sasa ni pasta jijini Los Angeles.

Christian amekuwa wakiugua tangu 2015 alipopatikana na uvimbe kwenye ubongo na kufanyiwa upasuaji mara ya kwanza nchini Amerika.Baada ya upasuaji huo, ambapo madaktari waliungama kuwa hangeendelea kuishi kwa muda mrefu, Christian aliendelea kuhudumiwa nyumbani.

Kwa bahati mbaya uvimbe huo ulitokea tena na akalazwa hospitalini kwa miezi kadhaa.The Longombas walihamia USA mwongo mmoja uliopita wakati umaarufu wao ulipokuwa umeshamiri zaidi Afrika Mashariki.Baadaye, Lovy aliamua kuokoka na kawa mhubiri jijini Los Angeles, Amerika.

Kaka hao wawili walitoka katika familia maarufu ya wanamuziki.Baba yao, Lovy Longomba Snr alikuwa mshirika katika bendi mashuhuri ya Lingala ya Super Mazembe, naye babu yao, Vicky Longomba alikuwa mshirika katika bendi ya TPOK Jazz.

You can share this post!

Kesi ya kumpinga Kavindu kuanza leo

Nyong’o apigwa kumbo na wandani wake wa zamani