Nyota wa zamani wa Barcelona atua Vissel Kobe ya Japan

Nyota wa zamani wa Barcelona atua Vissel Kobe ya Japan

Na MASHIRIKA

FOWADI wa zamani wa Stoke City na Barcelona, Bojan Krkic, amejiunga na kikosi cha Vissel Kobe cha Ligi Kuu ya Japan.

Bojan, 30, alichezea Stoke kati ya 2014 na 2019 baada ya kuanza kusakata soka ya kulipwa kambini mwa Barcelona.

Sogora huyo amekuwa bila klabu tangu aagane na Montreal Impact ya Major League Soccer (MLS) mnamo 2020.

Kufikia sasa, Vissel Kobe wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Japan (J1 League). Kikosi chao cha kwanza kinajumuisha pia kiungo wa zamani wa Barcelona, Andres Iniesta, 37, na beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen, 35.

Bojan amewahi pia kucheza AS Roma, AC Milan na Ajax.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kibarua kwa Rais Suluhu joto la kudai katiba mpya...

Ni uchaguzi wa masonko 2022