Nyuki wavamia kijiji na kuua mwanamke na kondoo wake

Nyuki wavamia kijiji na kuua mwanamke na kondoo wake

Na SAMMY KIMATU

MWANAMKE mwenye umri wa miaka 65 amefariki baada ya kushambuliwa na nyuki katika kijiji kimoja kaunti ya Machakos.

Kondoo wake watatu pia waliuawa na nyuki hao huku watu wengine kadhaa wakipata majeraha madogo.

Bi Muthoki Wambua alivamiwa na nyuki alipoenda kuokoa kondoo wake waliokuwa malishoni katika kijiji cha Kisekini, tarafa ya Mutituni.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa usalama eneo hilo, Bw Benson Him Nzyoki, hiki ni kisa cha nne cha wakazi wa kijiji hiki kuvamiwa na nyuki.

“Lakini wanakijiji waliofika katika eneo la kisanga walimlazimisha mamake kurudi nyumbani. Watu kadhaa walishambuliwa na nyuki hao waliokuwa na mzinga katikati ya mawe,’” Bw Him akasema.

 

You can share this post!

Mutua asisitiza alimwangusha Wavinya uchaguzini

Raia wa Argentina wagoma kulilia hali mbaya ya uchumi

adminleo