Nyuki wazua kizaazaa katika kituo cha mabasi cha Machakos

Nyuki wazua kizaazaa katika kituo cha mabasi cha Machakos

Na BENSON MATHEKA

KIZAZAA kilishuhudiwa jana mjini Machakos nyuki walipovamia mwanamke mara baada ya kushuka matatu kwenye kituo cha mabasi.

Walioshuhudiwa walisema mara baada ya mwanamke huyo kushuka gari lililokuwa limetoka Kaunti ya Kitui, nyuki walimvamia na kutua kwenye mkono wake wa kulia.’Aliangua kilio lakini nyuki hao hawakuondoka.

Askari walijaribu kuwaondoa wadudu hao lakini walimkwamilia na hakuna hata mmoja aliyeng’oka mkononi mwake,’ akasema dereva wa matatu katika kituo hicho.Umati mkubwa ulifika eneo la tukio kujionea kisa hicho ambacho wengi walisema kilitokana na uchawi.

Baadaye aliondolewa mahala hapo na mwendeshaji gari ambaye hakutambuliwa na wakaelekea kusikojulikana, hali iliyofanya wengi kushuku kuwa walikuwa pamoja.Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo walisema mkoba aliokuwa amebeba ulikuwa umejaa pesa na ndiposa nyuki ‘walitumwa’ kulinda asipokonywe.

Wengine walidai mkoba huo ulikuwa na mali ya wizi zikiwemo nguo na pesa.Mnamo Juni 4 mwaka huu, nyuki walivamia matatu za shirika la Kinatwa Sacco na kutatiza shughuli katika kituo hicho cha mabasi cha Machakos kwa saa kadhaa.

Wahudumu wa shirika hilo walidai nyuki hao walikuwa ‘wametumwa’ na kundi pinzani kuzuia magari hayo kubeba abiria, kwani hakuna mtu angeweza kuingia kwa hofu ya kushambuliwa na wadudu hao.

“Nyuki hao walikuwa wametumwa na wenzetu wa kundi pinzani ili kuvuruga biashara yetu. Hakuna hata gari moja ingeweza kuondoka, hivyo ikabidi abiria wapande matatu zao. Tukio hilo lilitatiza biashara yetu kwa saa kadhaa,” akasema mmoja wa wahudumu wa matatu za shirika hilo.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Ipo shida wauguzi kutofahamu lugha

300 wapewa vyeti vya uendeshaji boti

T L