Habari Mseto

Nzige sasa waanza kutafuna kahawa

February 25th, 2020 1 min read

Na GEORGE MUNENE

WAKULIMA wa kahawa katika kaunti ya Kirinyaga wamejawa na hofu baada ya nzige kuvamia mashamba kadhaa.

Wakulima hao wanasema kuwa nzige hao wameonekana katika vijiji vya Mukarara na Kiangecu katika eneo bunge la Gichugu na wanahofia kuwa watakula na kumaliza kahawa.

“Hadi sasa hakuna afisa mmoja wa serikali aliyetumwa kuchunguza hali ilivyo,” akasema Bw Josiah Muriithi, ambaye ni mkulima.

Mbunge wa eneo hilo,Bw Gichimu Githinji, alilaumu serikali ya kaunti kwa kuchukua muda mrefu kuwamaliza nzige hao.

“Wadudu hawa wameruka kutoka eneo la Gichungu hadi Mbeere siku tatu zilizopita na serikali haijafanya lolote ijapokuwa wana dawa za kuwanyunyizia,” akasema Bw Githinji.